Terms and Conditions-2026

VIGEZO NA MASHARTI MASHARTI YA M-GAS RESOURCES LIMITED YA UTOAJI HUDUMA YAKE YA LIPA KADRI UNAVYOTUMIA GESI NA KUUZA JIKO LA KUPIKIA LA STOVU Vigezo na masharti haya kama yalivyoelezwa katika waraka huu (Vigezo na Masharti) yanatumika kwa utoaji wa huduma ya lipa kadri unavyotumia gesi ya M-Gas Resources Limited, kampuni yenye dhima iliyo katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ofisi yake iliyosajiliwa inapatikana Plot No. 57, Ursino Estate, Uporoto Street (Bwawani), Postal code 14108, Mwananyamala Ward, Kinondoni District, P.O. Box: 75878, Dar es Salaam, Tanzania (M-Gas) kwa mtu anayeomba huduma hizi kutoka M-Gas (Mteja), kwa M-Gas kuuza na Mteja kununua Jiko la stovu (kama inavyoelezwa hapa chini).
  1. Tafsiri
1.1. Maneno yafuatayo yatakuwa na maana zifuatazo katika vigezo na Masharti haya: 1.1.1. Anwani ina maana ya anwani ya eneo Mteja alipo; 1.1.2. Mkataba lina maana kwa pamoja (i) mkataba ulioingiwa kati ya M-Gas na Mteja kama ilivyoainishwa katika waraka unaojulikana kama ‘Mkataba wangu na M-Gas’ na (ii) Vigezo na Masharti haya; 1.1.3. Taarifa Binafsi za Mteja ina maana iliyotolewa katika kifungu namba  8.2; 1.1.4. Sheria za Ulinzi wa Taarifa ina maana iliyotolewa katika kifungu namba 8.1; 1.1.3. Uwasilishaji bidhaa unakamilika pale M-Gas inapowasilisha jiko kwa Mteja kwa kutumia anwani ya Mteja. 1.1.4. Vifaa ina maana ya mtungi wa gesi, gesi iliyo katika mtungi, Jiko la stovu (ikiwa limetolewa kwa Mteja, na hadi wakati Jiko limekabidhiwa kwa Mteja kulingana na vifungu namba 6.2.3 au namba 6.3.3),mita , kadi ya kufungulia, na vitu vya ziada kama vile hozi ya kuunganisha na klipu ambazo hutolewa na M-Gas kwa Mteja kulingana na Mkataba na Masharti haya; 1.1.5. Malipo ya awali ya gesi ina maana iliyotolewa katika kifungu namba 5.5; 1.1.6. LPG ina maana ya gesi; 1.1.7 Tovuti ya M- Gas ina maana ya tovuti hii https://mgas.tz/terms; 1.1.7. Mfanyakazi wa M-Gas ina maana ya mfanyakazi, mshauri, wakala au ofisa wa M-Gas au mtu yeyote mshirika au mawakala wa M-Gas; 1.1.8. Kiasi kilichobaki ina maana ya kiasi cha bei ya Ununuzi na/au Kiasi kilichobaki cha ununuzi wa gesi ; 1.1.9. Kiasi cha GESI Kilichobaki ina maana iliyotolewa katika kifungu namba 5.6; 1.1.10. Kiasi cha Bei ya Ununuzi Kilichobaki ina maana iliyotolewa katika kifungu namba 6.5; 1.1.11. Siku ya Malipo ina maana iliyotolewa katika kifungu namba 6.3.1(b); 1.1.12. Malipo ya Awamu ya Bei ya Ununuzi ina maana iliyotolewa katika kifungu namba 6.3.1(b); 1.1.13. Huduma ya Matengenezo ina maana ya huduma ya matengenezo inayotolewa na M-Gas kulingana na kifungu namba 7; 1.1.14. Ada ya Huduma ya Matengenezo ina maana iliyotolewa katika kifungu namba 7.4; 1.1.15. Huduma ya Kubadilisha ina maana iliyotolewa katika kifungu namba 3.2.1; 1.1.16. Huduma ina maana ya utoaji wa Vifaa kwa mujibu wa kifungu namba 3 cha Vigezo na Masharti haya; 1.1.17. Jiko la stovu ina maana ya jiko jipya au lililotengenezwa la stovu linaloendana na matumizi ya Mteja na vifaa vilivyotolewa na M-Gas (na inajumuisha majiko yoyote mbadala yanayotolewa kwa mujibu wa kifungu namba 7.2 na namba 7.4 na haihusishi jiko lolote la stovu lililobadilishwa). 1.1.18. Tanzania ina maana ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 1.1.19. TSh. ina maana ya fedha halali ya Tanzania.
  1. Utoaji wa Vifaa na Huduma
    • Kabla ya Mkataba kuanza kutumika:
2.1.1. Mteja ataipatia kampuni ya M-Gas Anwani na namba yake ya simu ; 2.1.2.Kampuni ya M-Gas itamteua Mfanyakazi kumtembelea Mteja kwa kutumia Anwani aliyotoa ili kwenda kuona mahali ambapo vifaa vitawekwa na kutumika; 2.1.3. M-Gas itaamua ikiwa sehemu ambayo vifaa vitawekwa na kutumika inafaa au la. 2.1.4. M-Gas itaamua ikiwa mtu anayeomba huduma anafaa kuwa mteja wake au la.
  • Mteja atachukuliwa kuwa amekubali Mkataba, na marekebisho yatakayokuwa yanafanyika mara kwa mara:
2.2.1. Mteja atatia saini kwenye waraka unaojulikana kama ‘Mkataba Wako na M-Gas’; na 2.2.2. matumizi ya Mteja ya Huduma yoyote. 2.3 Baada ya M-Gas kuthibitisha kwamba vigezo vilivyowekwa katika kifungu namba 2.1 vimetimizwa: 2.3.1     Bila kuathiri matakwa ya kifungu namba 2.4 hapo chini kinachotoa muda wa kughairisha Mkataba, Mkataba huu utaanza kutumika na M-Gas itapanga utaratibu wa kuwasilisha Vifaa kwa Mteja kwa kutumia Anwani iliyotolewana mteja; 2.3.2     Mteja atafanya Malipo ya Awali ya gesi kulingana na kifungu namba 5.5; na 2.3.3     M-Gas itatoa Huduma kwa Mteja kulingana na Mkataba, na Vigezo na Masharti haya yatachukuliwa kuwa yamejumuishwa katika Mkataba na kumuwajibisha Mteja moja kwa moja, Isipokuwa, ili kuepuka shaka, M-Gas inaweza katika mazingira fulani kuamua kwamba vigezo vilivyoainishwa katika kifungu namba 2.1 vimetimizwa wakati sehemu au vigezo vyote havijatimizwa. 2.4. Bila kujali vifungu vilivyotangulia hapa juu, baada ya Mkataba huu kuanza kutumika, Mteja atakuwa na muda wa siku 10 wa kughairisha Mkataba. Katika kipindi cha kughairisha Mkataba, M-Gas haitompatia Mteja Vifaa vya aina yoyote issipokuwa tu pale Mteja atakapoomba kupewa Vifaa ndani ya kipindi cha kughairisha Mkataba. Ikitokea Mteja ameomba kupewa Vifaa kwenye kipindi cha kughairisha Mkataba, Mteja atapaswa kulipia Vifaa hivyo kwa mujibu wa Mkataba huu. Ili kuepua shaka, kipindi cha kughairi Mkataba kitaanza pale tu M-Gas itakapomtaarifu Mteja kuwa vigezo viliyoainishwa katika kifungu namba 2.1 vimetimizwa. 2.5. Mteja anakubali kwamba wakati wowote hatakuwa mmiliki au kudai kuwa na haki ya kisheria ya kumiliki Kifaa chochote kinachotolewa na M-Gas na kwamba kwa madhumuni yote ya Mkataba M-Gas itachukuliwa kama mmiliki wa kisheria wa vifaa vyote, bila ya kujali kwamba viko kwenye eneo la Mteja, na kwamba sharti hilo litatumika pia kwa Jiko hadi wakati ambapo M-Gas imelipwa na Mteja bei ya ununuzi wa Jiko la stovu.
  1. Wajibu wa M-Gas
3.1. M-Gas inaahidi kutoa Huduma kwa Mteja kama ifuatavyo: 3.1.1. kulingana na kifungu namba 3.2, M-Gas itatoa vifaa kwa kutumia Anwani iliyotolewa na Mteja, na, ikiwa inafaa, itaondoa mitungi ya gesi iliyotolewa na M-Gas ambayo tayari ipo kwa Mteja (Huduma ya Kubadilisha); 3.1.2. itatoa maelekezo na mafunzo kwa Mteja kuhusu jinsi ya kutumia vifaa kwa usalama, na iwapo mteja atazingatia, itasaidia kupunguza gharama; 3.1.3. itatoa namba ya huduma kwa Mteja kupiga simu ikiwa Mteja atashindwa kutumia kifaa kama ilivyokusudiwa au Mteja ana maswali au changamoto kuhusu Kifaa au Huduma; na 3.1.4. Itahakikisha kwamba Wafanyakazi wa M-Gas wanaomtembelea Mteja watakuwa na waraka unaowatambulisha kama wafanyakazi wa M-Gas (na kila Mfanyakazi wa M-Gas ataelekezwa kuonyesha waraka wa utambulisho pale mteja anapohitaji). 3.2. M-Gas inakusudia kuhakikisha kwamba Mteja ana mtungi wenye gesi wakati wote na kwamba Mfanyakazi wa M-Gas atakagua vifaa kila wakati anapokwenda kwa Mteja kubadili mtungi wa gesi. 3.3. M-Gas itajitahidi kuzingatia mahitaji yote ya leseni, afya na usalama ambayo yanaweza kutumika kwa Wafanyakazi wa M-Gas wanapomtembelea Mteja, lakini M-Gas haitawajibika chini ya Mkataba ikiwa, kwa sababu ya uzingatiaji huo inakiuka majukumu yake mengine chini ya Mkataba. 3.4. Ikiwa mabadiliko kwenye Huduma yanahitajika kutokana na mabadiliko ya sheria, taratibu au kanuni zinazotumika mara kwa mara au kukidhi matakwa ya usalama au mengine ya kiutendaji, M-Gas inaweza (kwa hiari yake ) kurekebisha Huduma kadri inavyoona inafaa ili kuzingatia mabadiliko ya sheria au kanuni zinazotumika au kukidhi usalama huo au matakwa mengine ya kiuendeshaji, au kwa kutoa taarifa kwa Mteja ya kuacha kutoa Huduma kwake. 3.5. M-Gas itatoa Huduma za matengenezo kwa Mteja kulingana na kifungu namba 7.
  1. Wajibu wa Mteja
4.1. Mteja anaahidi kwa M-Gas kwamba: 4.1.1. atatumia Vifaa na jiko la stovu (iwe limetolewa na M-Gas au mali ya Mteja) kulingana na maelekezo na mafunzo yaliyotolewa na M-Gas mara kwa mara, ambayo yanajumuisha (bila kikomo) masharti yafuatayo:
  1. a) atatumia tu vifaa vya kupikia chakula au vinywaji pekee;
  2. b) atatumia Vifaa katika eneo lenye hewa safi pekee;
  3. c) atatunza na kukilinda kifaa, ikihusisha (bila kikomo) kusafisha jiko baada ya matumizi na kufanya usafi wa kina angalau mara moja kwa wiki;
  4. d) hataruhusu mtoto au mtu mzima yeyote ambae hajapatiwa mafunzo na/au maelekezo yanayotolewa na M-Gas kwa ajili ya kutumia Kifaa;
  5. e) atatumia kifaa wakati kipo mbali na kitu chochote kinachoweza kuwaka; na
  6. f) atatumia jiko likiwa limewekwa juu kuliko mtungi wa gesi;
4.1.2. hatabadilisha, kurekebisha, kuchezea, kuharibu, kuhamisha au kutupa vifaa au sehemu ya kifaa, au kujaribu kukata mawasiliano ya sehemu yoyote ya kifaa; 4.1.3. hatauza, kukopesha, kukodisha, kutoa zawadi, kuchangia au kuhamisha kifaa au sehemu ya kifaa kwa mtu yeyote; 4.1.4. hatauza gesi kwa mtu mwingine yeyote (ikijumuisha, bila kikomo, kufanya kifaa kipatikane kwa matumizi yake); 4.1.5. hatatoa dhamana au kizuizi kingine chochote kuhusu kifaa au sehemu yake yoyote; 4.1.6. ataacha kutumia kifaa na Jiko ikiwa Mteja anashuku au anajua kwamba kifaa au jiko (au sehemu yoyote) halifanyi kazi kwa usahihi (ikiwa ni pamoja na, bila kikomo, ikiwa Mteja anaweza kupata gesi bila kuilipia) na kuripoti suala hilo katika Kampuni ya M-Gas haraka iwezekanavyo; 4.1.7.atakuwa kwenye eneo lake siku na wakati atakaoarifiwa na M-Gas ili kuwezesha Huduma ya Kubadilisha, atatoa Anwani kwa Wafanyakazi wa M-Gas kwa madhumuni ya kubadilisha mtungi wenye gesi, wafanyakazi watakagua na kujaribu kifaa cha kupikia, watajibu maswali ya mteja na kusaidia kazi nyingine zinazohusiana. Iwapo Mteja hatakuwa kwenye Anwani siku na wakati uliokubaliwa, Mteja lazima amjulishe M-Gas mara moja; 4.1.8. ataripoti katika Kampuni ya M-Gas ikiwa Mteja atapoteza au kuvunja kadi ya kufungulia au ikiwa kifaa kimehamishwa kutoka kwenye Anwani ya Mteja; 4.1.9.atatumia kifaa cha kupika mara kwa mara; 4.1.10. atashirikiana na M-Gas katika masuala yanayohusiana na Huduma, ikiwa ni pamoja na, bila kikomo, kurudisha kifaa katika mazingira yote pale ambapo M-Gas inahitaji Mteja kurudisha kifaa au sehemu ya kifaa, au kuruhusu kampuni ya M-Gas kuchukua kifaa kwa Mteja; 4.1.11. atatoa katika Kampuni ya M-Gas taarifa na nyaraka zote pale zinapohitajika kuhusiana na huduma, na kuhakikisha taarifa na nyaraka zilizotolewa ni sahihi na zimekamilika; 4.1.12. hatabadili eneo kutoka kwenye Anwani au nyumba ambayo Mteja aliiarifu M-Gas wakati au karibu na wakati M-Gas inawasilisha kifaa kwa Mteja; 4.1.13. hatabadili namba ya simu aliyoitoa katika kampuni ya M-Gas wakati au karibu na wakati M-Gas inawasilisha kifaa kwa Mteja; 4.1.14. hatatoa kwa mtu yeyote taarifa ya siri kuhusu biashara, mambo, wateja au wagavi wa M-Gas; na 4.1.15. hataruhusu mtu mwingine yeyote kufanya vitendo vyovyote vilivyopigwa marufuku na kifungu hiki 4.1. 4.2. Kwa kutumia kifaa, Mteja anaelewa kwamba kukiuka kifungu namba 4.1 kunaweza kusababisha hasara ya fedha na uharibifu kwa M-Gas. Ikiwa Mteja atakiuka kifungu namba 4.2 (ikiwa ni pamoja na, bila kikomo, kwa kuhamisha, au kuharibu kifaa au sehemu yeyote), kwa kufanya kitendo hicho Mteja anakubali kuilipa M-Gas akitakiwa kufanya hivyo kama itakavyoamuliwa na M-Gas na kutambuliwa kwa Mteja kwa wakati muafaka na bila taarifa kiasi sawa na thamani mbadala ya kifaa au sehemu husika kama fidia kwa vitendo vibaya vya Mteja huyo.
  1. Malipo ya gesi kwa M-Gas
5.1. Kwa kuzingatia utoaji wa Huduma wa M-Gas kwa Mteja, Mteja atailipa M-Gas kwa mujibu wa Vigezo na Masharti haya. 5.2. Mteja atafanya malipo kwa M-Gas kwa kutumia mixx by yas (namba ya malipo: 501166) au Airtel Money (chagua namba 44) na M-Gas itakubali malipo kutoka kwa Mteja kwa kutumia njia hizo tu. 5.3. Mteja hatahitaji kamwe kufanya malipo yoyote (kwa pesa taslimu au vinginevyo) moja kwa moja kwa Mfanyakazi yeyote wa M-Gas au kwa mtu mwingine au namba ya malipo yoyote, na hakuna Mfanyakazi wa M-Gas atamwomba Mteja kufanya malipo moja kwa moja kwake. Ikiwa Mteja ameombwa kufanya malipo moja kwa moja kwa Mfanyakazi wa M-Gas au kwa namba yoyote tofauti ya malipo, Mteja anatakiwa kukataa kufanya malipo hayo na kupiga simu mara moja kwa kutumia namba ya huduma kwa wateja ya M-Gas 800750382 kuelezea kilichotokea. 5.4. Mteja atanunua kutoka kwa M-Gas na M-Gas atamuuzia Mteja gesi katika kifaa kwa bei ya TSh.5,400 kwa kila kilogramu za gesi bila VAT. M-Gas ina weza kubadilisha bei ya gesi (ikiwa ni pamoja na, bila kikomo, kwa kutoa punguzo la bei ya gesi kwa Mteja) na itatoa taarifa ya mabadiliko ya bei na/au punguzo kwa Mteja kupitia Tovuti ya M-Gas na/au kwa ujumbe mfupi (SMS) au kupitia namba ya simu iliyotolewa na Mteja. 5.5. Mteja atafanya malipo ya awali ya Tsh. 5,000 kwa M-Gas kama malipo ya kwanza ya gesi (Malipo ya Awali ya Gesi). Kila wakati M-Gas inapopokea malipo ya gesi kutoka kwa Mteja, M-Gas itakata katika akaunti ya Mteja kiasi hicho, ambacho Mteja atatumia kununua gesi kwa kiwango kinachokubalika kama inavyoelezwa mara kwa mara katika kifungu namba 5.4. 5.6. Ikiwa Mteja atatambua au kushuku kwamba gesi inaweza kutolewa kwenye mtungi bila kufanya malipo, kwa mujibu wa kifungu namba 5.5, Mteja anapaswa kuitaarifu kampuni ya M-Gas mara moja. Ikiwa mtu aliyeidhinishwa na M-Gas atakubali vinginevyo, Mteja ataidai M-Gas kiasi sawa na gharama ya gesi iliyotolewa (kama itakavyoamuliwa na M-Gas kwa hiari yake) bila malipo (Kiasi cha gesi kilichobaki). 5:7. Ikiwa Mteja atapoteza kadi ya kufungulia, Mteja ataijulisha kampuni ya M-Gas mara moja. M-Gas inaweza kumtoza Mteja TSh. 1,500 kupata kadi mbadala ya kufungulia, na itatoa kadi mbadala kwa Mteja baada ya kupokea malipo ya kiasi hicho. 5.8. Pale ambapo M-Gas inachukua kifaa kutoka kwa Mteja, pia itakuwa na haki ya kuchukua Jiko. Kwa wakati huu, Mteja atakuwa na haki ya kubaki na Jiko ikiwa atailipa M-Gas Malipo yote ya Bei ya Ununuzi yaliyosalia na Kiasi chochote cha Bei ya Ununuzi kilichosalia, ambapo itamaanisha kwamba pale Mteja anapokamilisha ununuzi wa Jiko na kulipa bei kamili ya ununuzi, Jiko halitachukuliwa na M-Gas. Pale ambapo M-Gas inachukua Jiko kutoka kwa Mteja, Mteja hatakuwa na haki kurejeshewa fedha zozote ambazo tayari amelipa M-Gas kama bei kamili ya ununuzi wa Jiko hilo, na kampuni ya M-Gas haitawajibika kumrejeshea Mteja malipo yoyote ya aina hiyo. 5.9. M-Gas baada ya kutoa taarifa ya siku 5 kwa Mteja, inaweza: 5.9.1. kuchukua kiasi sawa na Kiasi kilichobaki kwa kukata kiasi hicho cha Shilingi za Tanzania ambazo zimelipwa na Mteja kununua gesi kutoka M-Gas ambazo zinabaki kama salio lililowekwa na Mteja kwenye akaunti yake na M-Gas; 5.9.2. pale ambapo kifungu cha 11.2 kinatumika, kurejesha gharama ya matengenezo au kubadili kifaa kwa kukata kutoka kwa kiasi chochote cha salio kilichowekwa na Mteja kwenye akaunti yake na M-Gas; na 5.9.3. kulipa dhima yoyote ya M-Gas kwa Mteja dhidi ya dhima yoyote ya Mteja kwa M-Gas, iwe dhima ya sasa au ya baadaye, imefutwa au haijafutwa, na ikiwa dhima inatokana na Mkataba au la.
  1. Uuzaji na Ununuzi wa Jiko
6.1. M-Gas itauza, na Mteja atanunua Jiko kulingana na kifungu hiki namba 6. 6.2. Pale ambapo Mteja anachagua kununua Jiko kwa kuchagua Chaguo A au C (Ununuzi wa moja kwa moja wa jiko jipya au lililotengenezwa ) katika Mkataba, basi: 6.2.1. baada ya kusaini Mkataba, Mteja atafanya malipo kwa M-Gas ya malipo ya bei ya ununuzi wa mara moja ya TSh. 70,000 (pamoja na VAT) kwa jiko jipya au TSh. 35,000 (pamoja na VAT) kwa jiko lililotengenezwa; 6.2.2. kihatarishi katika Jiko kitakuwa chini ya Mteja baada ya kuwasilishwa: 6.2.3. M-Gas itakuwa na haki na Jiko, na Jiko litakuwa chini ya Mteja baada ya (i) M-Gas kupokea kutoka kwa Mteja TSh. 70,000 ambapo Mteja ananunua jiko jipya au TSh. 35,000 ambapo Mteja ananunua jiko lililotengenezwa baada ya kulipa bei ya ununuzi wa mara moja, na (ii) Uwasilishaji wa Jiko la stovu kwa Mteja kufanyika; na 6.2.4. marejeleo ya kifaa katika Masharti haya yatachukuliwa kuwa ni pamoja na Jiko lililotolewa na M-Gas hadi wakati ambapo Mteja ana haki na jiko kulingana na kifungu namba 6.2.3. 6.3. Pale ambapo Mteja anachagua kununua Jiko kwa kuchagua Chaguo B au D (Ununuzi wa jiko jipya au lililotengenezwa kupitia malipo ya awamu) katika Mkataba, basi: 6.3.1. jumla ya kiasi kinacholipwa na Mteja kitakuwa:
  1. 7,500 kwa Jiko jipya (pamoja na VAT) au TSh. 3,750 kwa jiko lililotengenezwa ambayo italipwa na Mteja kwa M-Gas baada ya kusaini Mkataba; na
 
  1. kwa mujibu wa kifungu cha 7, malipo ya ya awamu ya bei ya ununuzi ya TSh. 750 (pamoja na VAT) (kila moja, Awamu ya Bei ya Ununuzi) yatalipwa na Mteja kwa M-Gas kila wiki hadi wakati Mteja atapokuwa amelipa TSh. 85,500 (pamoja na VAT) kutoka malipo ya awamu ya Bei ya Ununuzi yote ya jiko jipya au TSh. 42,750 (pamoja na VAT) kwa jumla kutoka malipo ya awamu ya Bei ya Ununuzi ya jiko jipya. Mteja atalipa Malipo ya Awamu ya Bei ya Ununuzi Jumatatu (au siku nyingine ya wiki kama ilivyoarifiwa na M-Gas kwa Mteja) ya kila wiki (Siku ya Malipo);
6.3.2. dhamana katika jiko itakuwa chini ya mteja baada ya kuwasilishwa; 6.3.3. M-Gas itakuwa na haki na Jiko, na Jiko litakuwa chini ya Mteja mara baada ya M-Gas kupokea kutoka kwa Mteja (i) jumla ya TSh. 85,500 kwa jiko jipya au (ii) jumla ya TSh. 42,750 kwa jiko lililotengenezwa kutoka kwa Mteja kupitia malipo ya bei ya awali ya ununuzi na malipo ya awamu ya Bei ya ununuzi na (iii) malipo yote yanayopaswa kulipwa na Mteja kulingana na kifungu namba 7; na 6.3.4. marejeleo ya kifaa katika Masharti haya yatachukuliwa kuwa ni pamoja na Jiko lililotolewa na M-Gas hadi wakati ambapo Mteja ana haki na jiko kulingana na kifungu namba 6.2.3. 6.4. Mteja atalipa malipo ya awali ya bei ya ununuzi na kila Malipo ya Bei ya Ununuzi kwa M-Gas kwa kutumia Mixx by yas (namba ya malipo: 501166) au Airtel Money (chagua namba 44). 6.5. Ikiwa Mteja atashindwa kufanya malipo kamili ya awamu ya Bei ya Ununuzi ifikapo saa 23:59 katika Siku ya Malipo katika wiki yoyote, M-Gas itakata kiasi ambacho ni sawa na kiasi cha Malipo ya awamu ya Bei ya Ununuzi kutoka ama katika kiasi kinachofuata ambacho Mteja atalipa kwa M-Gas kama gharama ya gesi au kutoka kwenye salio la Mteja ambalo M-Gas inashikilia katika akaunti ya Mteja huyo kwa wakati huo au vyote kwa pamoja. M-Gas itatumia kiasi kilichokatwa ili kutoa malipo ya kiasi kilichobaki cha Malipo ya Awamu ya Bei ya Ununuzi. Ikiwa kiasi ambacho Mteja hulipa kama gharama ya gesi au ikiwa kiasi cha salio la Mteja ambacho M-Gas anashikilia katika akaunti ya Mteja huyo kwa wakati huo ni chini ya thamani ya kiasi kilichobaki cha Awamu ya Bei ya Ununuzi, basi M-Gas itatoa kiasi chote (kama kipo) kinacholipwa na Mteja kama gharama ya gesi na salio lote la Mteja (kama lipo) ambalo M-Gas inashikilia katika akaunti ya Mteja huyo kwa wakati huo, na M-Gas itatumia kiasi ilichokata kulipa kiasi kilichobaki cha malipo ya awamu ya bei ya ununuzi (hadi kufikia thamani ya kiasi kilichokatwa), na Mteja ataidai M-Gas kiasi kingine kilichobaki cha malipo ya awamu ya Bei ya Ununuzi (Kiasi cha Bei ya Ununuzi Kilichobaki). 6.6. Pale ambapo, wakati wowote Malipo ya Bei ya Ununuzi yanatakiwa kutolewa na Mteja, Mteja huyo anadaiwa Kiasi cha Bei ya Ununuzi na M-Gas, Mteja atatakiwa kuilipa kampuni ya M-Gas kiasi sawa na Malipo ya awamu ya Bei ya Ununuzi na Kiasi cha Bei ya Ununuzi. 6.8. Vigezo hivyo vinaelezwa na Sheria ya Uuzaji wa Bidhaa (Sura 214), kwa kiwango kamili kinachoruhusiwa na sheria, havimo kwenye Mkataba. 6.9. Ikiwa Mteja anatumia jiko ambalo halijatolewa kwa Mteja na M-Gas, Mteja anakubali kutumia na kulitunza jiko hilo kulingana na maelekezo ya matumizi (na kwa namna yoyote hataruhusu watoto kutumia jiko hilo) na M-Gas haitawajibika kwa Mteja kuhusiana na matumizi au kuvunjika au kushindwa kufanyakazi kwingine kwa jiko hilo.
  1. Huduma ya Matengenezo ya Jiko
7.1. M-Gas itatoa Huduma ya matengenezo kwa Wateja ambao wameamua kununua Jiko kwa kuchagua Chaguo A (Ununuzi wa moja kwa moja wa jiko jipya), Chaguo B (Ununuzi wa jiko jipya kupitia malipo ya awamu), Chaguo C (Ununuzi wa moja kwa moja wa jiko lililotengenezwa), au Chaguo D (Ununuzi wa jiko lililotengenezwa kupitia malipo ya awamu) kiwango cha juu mara mbili katika kipindi cha miaka miwili kuanzia tarehe ambayo Mteja kwanza anakubali kununua Jiko kutoka kwa M-Gas, katika kila jambo kulingana na kifungu hiki cha 7. Huduma ya matengenezo haipatikani kwa Wateja hao ambao wameamua kutumia jiko kutoka kwa mtu mwingine tofauti na M-Gas. 7.2. Ikiwa Jiko jipya au lililotengenezwa litakuwa na hitilafu yoyote na Mteja kuitaarifu kampuni ya M-Gas ndani ya mwezi mmoja kuanzia tarehe ambayo Mteja amekubali kwanza kununua Jiko kutoka M-Gas, kampuni ya M-Gas italichukua Jiko lenye hitilafu kutoka kwa Mteja na kumpatia Jiko mbadala linalofanya kazi , na hakuna Ada ya Huduma ya matengenezo itakayolipwa. 7.3. Ikiwa Jiko jipya au lililotengenezwa lina hitilafu yoyote baada ya mwezi mmoja kupita tangu tarehe ambayo Mteja kwanza anakubali kununua Jiko kutoka kampuni ya M-Gas, Mteja ataitaarifu kampuni ya M-Gas juu ya hilafu hiyo, ambapo M-Gas itatoa Huduma ya matengenezo kwa mujibu wa vifungu vifuatavyo vya kifungu hiki namba 7. 7.4. Pale ambapo Mteja anaijulisha kampuni ya M-Gas kwamba Jiko jipya au lililotengenezwa alilopatiwa lina hitilafu baada ya mwezi mmoja kupita tangu tarehe ambayo Mteja anakubali kununua Jiko kutoka M-Gas, M-Gas italichukua Jiko lenye hitilafu kutoka kwa Mteja na itatoa Jiko jipya au lililotengenezwa (kadri hali itakavyokuwa) kwa Mteja ambapo Mteja atawajibika kulipa ada ya Huduma ya matengenezo ya Tsh. 4,500 (pamoja na VAT) (Ada ya Huduma ya Matengenezo). 7.5. Pale ambapo Mteja ameamua kununua Jiko kwa kuchagua Chaguo A au C (Ununuzi wa moja kwa moja wa jiko jipya au lililotengenezwa) katika Mkataba, basi Mteja atalipa Ada ya Huduma ya matengenezo kwa awamu moja, ambayo italipwa mara moja na ambayo lazima ilipwe kikamilifu na Mteja kabla ya M-Gas kutoa Huduma ya matengenezo. 7.6. Pale ambapo Mteja ameamua kununua Jiko kwa kuchagua Chaguo B au D (Ununuzi wa jiko jipya au lililotengenezwa kupitia malipo ya awamu) katika Mkataba, basi Mteja atalipa Ada ya Huduma ya matengenezo kwa awamu nane jumla Tsh. 562.50 kila moja. Pande husika zinakubali kwamba wakati wowote ambapo Ada ya Huduma ya matengenezo au sehemu yake yoyote imebakia, basi kiasi chote kilichopokelewa na M-Gas kutoka kwa Mteja tofauti na michango ya gesi kitachukuliwa kama malipo na yatatumika kama Ada ya Huduma ya matengenezo kwa kipaumbele kwa malipo ya Awamu yoyote ya Bei ya Ununuzi. 7.7. Katika kila hali, Mteja atalipa Ada ya Huduma ya matengenezo kwa kutumia Mixx by yas (namba ya malipo: 501166) au Airtel Money (chagua namba 44).
  1. Taarifa za Mteja
8.1. Ili kuiwezesha M-Gas kutimiza majukumu yake ya kimkataba chini ya Mkataba au kwa madhumuni mengine yoyote halali kama ilivyoagizwa na Sheria ya Ulinzi wa Taarifa binafsi ya mwaka 2022, kanuni zozote hapa chini na sheria nyingine zozote zinazotumika (Sheria za Ulinzi wa Taarifa), M-Gas inahitaji kuchakata Taarifa binafsi za Mteja (zilizoelezwa hapa chini) kwa madhumuni ambayo ni pamoja na yafuatayo: 8.1.1. kuchakata maombi ya bidhaa na huduma, kufanya malipo, miamala, kuchukua vifaa na Majiko kutoka kwa Mteja au mawakala wa M-Gas walioidhinishwa pale inapohitajika, na kukamilisha maelekezo au maombi ya Mteja; 8.1.2. kutoa bidhaa na huduma kwa Mteja, ikiwa ni pamoja na Huduma ya Matengenezo, Huduma ya kubadilisha vifaa na Huduma zingine; 8.1.3. kutathmini kufaa kwa bidhaa na huduma zingine; 8.1.4. tathmini ya mkopo, ikiwa ni pamoja na kufanya ukaguzi wa mkopo na kuweka ukomo wa mkopo na kupata taarifa za mkopo; 8.1.5. kutangaza bidhaa, huduma mpya na zilizopo; 8.1.6. uchanganuzi wa biashara, utafiti, na madhumuni ya takwimu; 8.1.7. kuzingatia matakwa ya kisheria, serikali au udhibiti au kwa matumizi ya washauri wa kisheria wa M-Gas kuhusiana na mashauri yoyote ya sasa au yanayotarajiwa ya kisheria; 8.1.8. Ufuatiliaji wa kutumia CCTV wa majengo ya biashara ya M-Gas ili kuyafanya kuwa salama; 8.1.9. kutoa taarifa ya siri (ambayo haina taarifa yoyote inayoweza kumtambua Mteja kama mtu binafsi) kwa wahusika wengine ikiwa ni pamoja na kwa madhumuni ya utafiti na kisayansi; 8.1.10. kuwezesha M-Gas na mawakala kutathmini, kufuatilia na kupima upunguzaji wa uzalishaji, pamoja na haki nyingine zozote zinazohusiana na bidhaa za mazingira, ambazo zinaweza kupatikana kutokana na matumizi ya Kifaa; na 8.1.11. usimamizi wa majukwaa ya mtandaoni au tovuti za M-Gas. 8.2. Hapa Mteja anatoa idhini yake kwa M-Gas (i) kukusanya, kuchakata na kuhifadhi taarifa za Mteja ikiwa ni pamoja na taarifa zake binafsi (Taarifa Binafsi za Mteja) na kwa M-Gas (ii) kuteua wachakataji wa kuchakata Taarifa Binafsi za Mteja ili kutimiza au kutekeleza vizuri majukumu yake ya kimkataba na Mteja na pia kwa madhumuni yoyote halali ya kibiashara. 8.3. Mteja ana haki zake chini ya Sheria za Ulinzi wa Taarifa na M-Gas itahakikisha kwamba ukusanyaji, uchakataji, uhifadhi na uhamishaji wa taarifa binafsi unafanyika kwa mujibu wa Sheria za Ulinzi wa Taarifa na Sera ya Ulinzi wa Taarifa ya M-Gas ambayo inapatikana katika Tovuti ya M-Gas. 8.4. M-Gas inaweza kuchagua kuteua wachakataji wasaidizi na itafanya mchakato huu kulingana na Sheria za Ulinzi wa Taarifa. Orodha ya awali ya wachakataji wasaidi walioidhinishwa inapatikana kwenye Tovuti ya M-Gas ambayo itahuishwa. Iwapo M-Gas itateua wachakkataji wasaidizi wa ziada au mbadala itatakiwa kuhuisha tovuti yake ipasavyo na Mteja atakuwa na haki ya kupinga uchakataji unaofanywa na wachakataji wasaidizi wa ziada au mbadala kwa mujibu wa Sheria za Ulinzi wa Taarifa (ikiwa Taarifa Binafsi za Mteja zinashughulikiwa kwa madhumuni ya matangazo). Ikiwa Mteja atazuia uwezo wa mchakataji na/au njia ya kuchakata taarifa yake, M-Gas ina haki ya kusitisha kutoa Huduma na inaweza, kwa kutoa taarifa kwa Mteja, kusitisha uhusiano wake na Mteja na kuchukua hatua zote muhimu kwa M-Gas kurejesha pesa zozote zinazodaiwa na M-Gas pamoja na Vifaa na Jiko.   8.5. Mteja anakubali kwamba M-Gas inaweza kuhifadhi na/au kuhamisha Taarifa zake Binafsi nje ya Tanzania na hivyo Mteja anakubali M-Gas kuhifadhi na/au kuhamisha Taarifa zake Binafsi nje ya Tanzania kwa mujibu wa Sheria za Ulinzi wa Taarifa. 8.5 Pale ambapo Mteja anapotoa taarifa binafsi ya mtu mbadala wa kuwasiliana na M-Gas, Mteja anathibitisha kwamba (i) ameidhinishwa na mtu huyo mbadala kutoa taarifa zake binafsi kwa M-Gas kwa madhumuni ya kutimiza majukumu yake au kutekeleza haki zake chini ya Mkataba, (ii) mtu mbadala anajua kwamba madhumuni ya Mteja kutoa taarifa binafsi za mtu mbadala kwa M-Gas ni kama ilivyoainishwa katika kifungu namba 8.1 na (iii) mtu mbadala wa kuwasiliana na kampuni ya M-Gas amemthibitishia Mteja kwamba anakubali taarifa zake binafsi kutumiwa na M-Gas.  
  1. Ukomo wa Dhima
9.1. M-Gas haitawajibika kwa Mteja, iwe kwa mkataba au vinginevyo, kwa kukiuka wajibu wa kisheria au vinginevyo kutokea chini ya Masharti haya au vinginevyo kuhusiana na uhusiano wake na Mteja kupoteza faida au akiba inayotarajiwa, hasara ya mauzo au biashara, hasara ya mikataba kupoteza au uharibifu wa nia njema, au hasara yoyote isiyo ya moja kwa moja au inayoweza kujitokeza. 9.2. M-Gas haitawajibika kwa Mteja, kwa kiwango cha juu kinachoruhusiwa na sheria, kwa hasara yoyote au gharama zinazotokana au kuhusiana 9.2.1 Mteja anayetumia, au kuruhusu mtu mwingine kutumia kifaa au Jiko (au sehemu yake yoyote ) tofauti kulingana na maelekezo na/au mafunzo ambayo amepatiwa; 9.2.2. Mteja vinginevyo kukiuka Mkataba (ikiwa ni pamoja na majukumu yaliyomo katika kifungu namba 4). 9.3. Jumla ya dhima ya M-Gas kwa Mteja, iwe katika mkataba au vinginevyo, kwa kukiuka wajibu wa kisheria au vinginevyo chini ya Masharti haya au vinginevyo kuhusiana na uhusiano wake na Mteja, itakoma katika thamani ya jumla ya malipo ya gesi yaliyotolewa na Mteja kwa M-Gas kwa kipindi cha miezi sita kabla ya tarehe ya taarifa ya madai yaliyowasilishwa na Mteja kwa M-Gas.
  1. Tukio Lisilozuilika (Force Majeure) na mambo yaliyo nje ya uwezo wa pande zote mbili
10.1. Kwa madhumuni ya Masharti haya, Tukio Lisilozuilika linamaanisha hali yoyote ambayo haiwezi kudhibitiwa na upande wowote kwenye Mkataba huu, ikiwa ni pamoja na vitendo vya Mungu, mafuriko, ukame, tetemeko la ardhi au janga lingine la asili; janga au mlipuko wa magonjwa; shambulio la kigaidi, vita vya wenyewe kwa wenyewe, ghasia za wenyewe kwa wenyewe au fujo, vita, tishio au maandalizi ya vita, migogoro ya kutumia silaha, kuwekewa vikwazo, au kuvunja uhusiano wa kidiplomasia; uchafuzi unaosababishwa na nyuklia, kemikali au kibaiolojia au kuongezeka kwa sauti; sheria yoyote au hatua yoyote iliyochukuliwa na mamlaka ya serikali au ya umma, ikiwa ni pamoja na kuweka kizuizi cha kuuza bidhaa nje au kuagiza nje, marufuku, au kushindwa kutoa idhini muhimu, leseni au idhini; kuanguka kwa majengo, moto, mlipuko au mgogoro wowote wa biashara, migomo, migomo ya viwandani au kufungwa; hatua za viwandani na wagavi au wakandarasi wadogo; na kutatisha au kushindwa kwa huduma mawasiliano ya simu na /au huduma za fedha za simu. Kwa madhumuni ya Masharti haya, upande wa utakaoathiriwa na Tukio Lisilozuilika utajulikana kama “Upande Ulioathiriwa”. 10.2. Ikiwa upande wowote umezuiwa au kucheleweshwa kutekeleza majukumu yake yoyote kama ilivyoainishwa katika Masharti haya kutokana Tukio Lisilozuilika, upande huo hautakuwa umekiuka Masharti haya na hautawajibishwa kwa kushindwa kutekeleza majukumu hayo. 10.3. Baada ya kutokea kwa Tukio Lisilozuilika, Upande Ulioathiriwa utafanya jitihada za kuujulisha upande mwingine kuhusu Tukio hilo kwa njia yoyote ya maandishi au kieletroniki ila M-Gas itapaswa kutoa taarifa ya Tukio Lisilozuilika kwa njia televisheni, redio, gazeti au kwa kuweka taarifa kwenye Tovuti ya M-Gas. Upande Ulioathiriwa utaonesha katika taarifa yake Tukio Lisilozuilika linategemewa kudumu kwa muda gani na athari za Tukio hilo katika uwezo wa Upande Ulioathiriwa kutekeleza majukumu yake yoyote chini ya Masharti haya. Vilevile, Upande Ulioathiriwa utachukua hatua za makusudi ili kupunguza athari za Tukio hilo kwa ajili ya utekelezaji wa majukumu yake chini ya Masharti haya. 10.4. Ikiwa Tukio Lisilozuilika linazuia au kuchelewesha utekelezaji wa majukumu ya Upande Ulioathiriwa kwa kipindi endelevu cha zaidi ya wiki mbili, Upande Ulioathiriwa unaweza kusitisha uhusiano wake na upande mwingine kwa kutoa taarifa.
  1. Kuvunja Mkataba
11.1. Mteja anaweza kusitisha uhusiano wake na M-Gas wakati wowote kwa kurudisha Vifaa katika kampuni ya M-Gas kwa kutumia anwani ya M-Gas wakati wa saa za kazi (ilimradi mfanyakazi aliyeidhinishwa wa M-Gas amekubali kupokea vifaa hivyo) au namna nyingine iliyokubaliwa na M-Gas. Kifaa chochote kinachorudishwa katika kampuni ya M-Gas lazima kiwe safi, kimetunzwa vizuri na kiwe katika hali nzuri ya kufanya kazi. 11.2. Ikiwa Kifaa chochote kilichorejeshwa na Mteja katika kampuni ya M-Gas baada ya kusitishwa kwa uhusiano wa Mteja na M-Gas hakifai tena kutumiwa na Mteja mwingine (kama itakavyoamuliwa na M-Gas kwa hiari yake kabisa), Mteja atawajibika kwa M-Gas kwa gharama ya matengenezo au kutoa Kifaa mbadala , makato kiasi kutokana na kuchakaa au uharibifu wa kifaa (kama upo). 11.4. Baada ya kutoa taarifa ka mteja M-Gas inaweza, wakati wowote , kuacha kutoa Huduma na (ama yenyewe au kupitia wakala) kuchukua hatua muhimu za kurejesha Kifaa kutoka kwa Mteja. 11.3. Ikiwa wakati wowote: 11.3.1. Mteja anakiuka wajibu wake kama ilivyoainishwa katika Mkataba; 11.3.2. utekelezaji wa M-Gas wa Huduma zake kulingana na Mkataba unazuiwa au kucheleweshwa na kitendo chochote au kutolewa kwa Mteja; au 11.3.3. Mteja hawezi kulipa madeni yake kama inavyostahili au ametangazwa kufilisika, au maombi yamewasilishwa mahakamani au amri imetolewa au hatua nyingine yoyote imechukuliwa dhidi ya Mteja, M-Gas inaweza kusitisha kutoa Huduma na inaweza, kwa kutoa taarifa kwa Mteja, kusitisha uhusiano wake na Mteja na kuchukua hatua zote muhimu kwa M-Gas za kurejesha pesa zozote zinazodaiwa na M-Gas pamoja na Vifaa na Jiko kutoka kwa mteja. 11.4. Baada ya uhusiano kati ya M-Gas na Mteja kusitishwa kwa mujibu wa Masharti haya, Mteja atarudisha Vifaa mara moja kwa M-Gas, au kupanga utaratibu wa M-Gas kuchukua vifaa au vinginevyo vifaa kurudishwa katika kampuni ya M-Gas.
  1. Umiliki wa Vibali vya “Carbon Credits”
Ninaelewa kwamba mapato yanayotokana na uuzaji wa vibali vya ”Carbon Credits” hutumiwa kusaidia ununuzi na usambazaji wa vifaa. Kwa mujibu wa sheria za Tanzania za ununuzi na usambazaji wa “carbon credits”, Mteja anakubali kuhamisha kwenda kwa M-Gas, haki zake zote zinazohusiana na kupunguza uzalishaji wa hewa ya ukaa (carbon), pamoja na bidhaa nyingine yoyote inayohusiana na mazingira iliyopatikana kutokana kwa matumizi ya Vifaa.
  1. Jumla
13.1. Uhusiano kati ya M-Gas na Mteja ni wa binafsi kwa Mteja, na Mteja hawezi kugawa, kuhamisha, kuweka rehani, kutoza, kutoa kazi kwa mtu mwingine, kukabidhi, kutangaza uaminifu juu au kushughulika kwa njia nyingine yoyote na haki na majukumu yake yoyote chini ya Masharti haya. M-Gas inaweza wakati wowote kugawa, kuweka rehani, kutoza, kutangaza uaminifu juu au kushughulika kwa njia nyingine yoyote na haki zake zozote au zote katika uhusiano kati ya M-Gas na Mteja au chini ya Masharti haya, na inaweza kusaini mkataba wowote wa majukumu yake kama ilivyoainishwa katika Masharti haya. 13.2. M-Gas inaweza kurekebisha vigezo vya Masharti haya wakati wowote, na Mteja atachukuliwa kuwa anaelewa na amekubali Masharti yoyote yaliyorekebishwa kwa kuendelea kutumia Huduma baada ya marekebisho, ili mradi tu marekebisho hayo yawe yamepitishwa na mamlaka husika ikiwemo Tume ya Ushindani ya Tanzania. 13.3. Endapo kutajitokeza mgogoro au kutofautiana kati ya Masharti haya na waraka ujulikanao ‘Mkataba wangu na M-Gas’, Masharti haya yatatumika. 13.4. Kuondolewa kwa haki au suluhu yoyote chini ya Mkataba au kwa sheria kunatumika tu ikiwa kumefanywa kwa maandishi na hakutachukuliwa kama kuondolewa kwa haki au suluhu yoyote inayofuata. Kushindwa au kuchelewa kwa M-Gas kutumia haki yoyote au suluhisho iliyotolewa chini ya Mkataba au kwa sheria haitajumuisha msamaha wa haki hiyo au haki nyingine yoyote au suluhu, wala haitazuia au kuzuia matumizi yoyote zaidi ya haki hiyo au haki nyingine yoyote au suluhisho. Hakuna utekelezaji mmoja au sehemu ya haki yoyote au suluhisho lililotolewa chini ya Masharti haya au kwa sheria utakaozuia utekelezaji zaidi wa haki hiyo au haki nyingine yoyote au suluhisho. 13.5. Ikiwa kifungu chochote au sehemu ya Mkataba au Masharti haya ni batili, haramu au hayatekelezeki, itachukuliwa kuwa kimefutwa, lakini haitaathiri uhalali na utekelezaji wa Mkataba uliobaki au Masharti haya. Vilevile, ikiwa kifungu chochote au sehemu ya Mkataba au Masharti haya itaonekana kufutwa, matumizi yoyote yanayoendelea ya Mteja anayepatiwa Huduma yatachukuliwa kuwa makubaliano na kwamba kifungu hicho kinachukuliwa kubadilishwa na kifungu ambacho, kwa kiwango kikubwa , kinafanikisha matokeo ya kibiashara yaliyokusudiwa ya kifungu halisi. 13.6. Mkataba unaunda makubaliano kati ya M-Gas na Mteja na unachukua nafasi na inazima makubaliano ya awali, ahadi, uhakikisho, dhamana, uwakilishi na uelewa wote kati yao wa maandishi au mdomo kuhusiana na mada husika. 13.7. Mkataba unaweka uhusiano kati ya M-Gas na Mteja, na uhusiano huo hautengenezi haki yoyote kwa mtu mwingine yeyote kutekeleza vifungu vya Masharti haya. Bila kujali kwamba M-Gas inaweza kuwa sio mmiliki halali wa Kifaa, Mteja anakubali kwamba, kwa kiwango ambacho Kifaa hakimilikiwi kisheria na M-Gas, M-Gas imeidhinishwa na mmiliki husika wa kisheria wa Kifaa hicho kupeleka Kifaa hicho kwa Mteja na imeidhinishwa kuchukua Kifaa hicho kwa mujibu wa Masharti haya. 13.8. Mkataba na mgogoro au madai yoyote (ikiwa ni pamoja na migogoro au madai yasiyo ya mkataba) yanayotokana au kuhusiana na Mkataba au suala au utokeaji wake yatasimamiwa na kutafsiriwa kwa mujibu wa sheria za Tanzania. 13.9. M-Gas na Mteja wanakubaliana kwamba mahakama za Tanzania zitakuwa na mamlaka ya kipekee ya kutatua mgogoro au madai yoyote (ikiwa ni pamoja na migogoro au madai yasiyo ya mkataba) yanayotokana au kuhusiana na Mkataba au suala au utokeaji wake.